Jumapili 4 Mei 2025 - 08:15
Hawza ya Qum; Muunganiko ulio na miaka takriban Elfu katika elimu ya kiislamu na ulimwengu wa zama hizi

Hawza ya Qum ikiwa ni urithi wa zaidi ya miaka 1200, siyo tu mojawapo ya vituo vikuu vya uzalishaji na usambazaji wa elimu ya Kiislamu, bali pia kwa kulea wanafunzi wa kimataifa na kuwaunganisha, imekuwa na athari kubwa katika mchakato wa kufikisha fikra ya Kiislamu duniani kote.

 Shirika la Habari la Hawza,/ Wakati mwingine taasisi ya kielimu hufanya kazi zaidi ya darasa, na kituo cha kidini hutenda kazi zaidi ya mipaka ya hawza;  na wakati mwingine, elimu kinyume na matarajio hugeuka kuwa chombo cha kubadilisha tamaduni na jamii.

Hawza ya Qum siyo tu kituo cha elimu na utafiti, bali ni harakati ya kifikra iliyonyooka katika muktadha wa historia, na leo hii inazidi kusonga mbele katika ulimwengu tulio nao.

Hawza hii imejengwa katika mfumo wa elimu tangia na karne za mwanzo za kiislamu, ambapo mtandao wa shule na vituo vya kielimu ulianzishwa. Kuanzia Baghdad na Nishabur hadi Najaf na Qum, hawza zimeweza kuigeuza elimu ya Kiislamu katika nyanja mbali mbali kama vile ijtihadi, falsafa, fiqhi, Kalam, na Usuli. Qum, katika karne zilizopita imewasilisha sura mpya ya urithi huu wa kihistoria. Hawza hii haijashughulika tu na kulea wanazuoni na mujtahidina tu, bali pia kwa kuunda daraja la kuunganisha fikra ya Kiislamu na mahitaji ya kisasa ya jamii, imejigeuza kuwa mchezaji hai katika medani ya kimataifa.

Nafasi ya Hawza ya Qum katika Kusambaza elimu ya Kiislamu na Kulea Wanafunzi wa Kimataifa

Qum leo hii siyo tu mji wa kidini, bali ni kituo cha kimataifa kwa upande wa elimu ya Kiislamu.

Jami‘at al-Mustafa al-‘Alamiyyah, mojawapo ya taasisi muhimu zilizo chini ya hawza ya Qum, imewafundisha zaidi ya wanafunzi 50,000 kutoka nchi 122 duniani kote, ambao leo hii ni mabalozi wa fikra ya Kiislamu katika jamii zao. Wengi wao, baada ya kurejea makwao, wamekuwa wakufunzi wa vyuo vikuu, wahubiri wa dini na wasomi wa kidini wanaotangaza maarifa ya Kiislamu na kutekeleza mfumo wa fikra ya hawza katika maeneo mbalimbali ya kijiografia.

Hawza ya Qum siyo tu katika fiqhi na usuli, bali pia katika falsafa ya Kiislamu, sheria ya Kiislamu na tafsiri ya Qur’ani imekuwa na mchango mkubwa. Katika miongo ya hiv karibuni, tafiti zilizofanyika Qum kupitia tafsiri na uchapishaji wa kimataifa, zimekuwa mojawapo ya vyanzo vikuu vya elimu ya Kiislamu duniani.

Katika mwelekeo wa kuhakiki upya na mabadiliko ya elimu ya Kiislamu, Hawza ya Qum imekuwa daima katika njia ya uhakiki upya na mabadiliko ya elimu ya Kiislamu. Mfumo wa ijtihadi katika hawza hii, ukiwa mojawapo ya nyenzo za fikra ya Shia, umeweza kuimarisha mwingiliano wa kielimu na wa kimadhehebu.

Baadhi ya juhudi muhimu za hawza ya Qum katika kueneza elimu ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Kuanzisha taaluma mpya: Masomo ya Kiislamu linganishi, sheria ya kimataifa ya Kiislamu, na falsafa ya maadili ya kimataifa.

Mwingiliano wa kitamaduni: Ushirikiano wa kielimu na vyuo vikuu maarufu kama vile Al-Azhar ya Misri na taasisi za utafiti za Ulaya.

Upanuzi wa mijadala ya kielimu: Ushiriki wa wanazuoni wa hawza katika makongamano ya kimataifa na kushiriki mijadala ya kidini ya kimadhehebu. Hatua hizi zimeifanya hawza ya Qum kutoka kuwa kituo cha kisunnah na kuwa mchezaji mwenye athari katika mazungumzo ya kidini na kifalsafa duniani.

Nafasi ya Wanawake katika Kuendeleza elimu Kiislamu: Kuunda upya nafasi ya kielimu kwa wanawake

Kinyume na mtazamo wa kisunna, nafasi ya wanawake katika hawza ya Qum haijabaki tu katika elimu ya kidini. Leo hii, wanafunzi wa kike wa dini wanashiriki siyo tu katika mchakato wa ijtihadi na tafiti za fiqhi, bali pia wamekuwa na athari katika nyanja za vyombo vya habari na utamaduni.

Jami‘at az-Zahra (as) ni mojawapo ya taasisi za kielimu zilizo chini ya hawza ya Qum, imeweka mazingira ya kuendeleza nafasi ya mwanawake katika fikra ya Kiislamu. Taasisi hii siyo tu kituo cha elimu, bali ni chombo huru cha utafiti ambacho kimewawezesha wanafunzi wa kike kufanya tafiti za Kiislamu katika ngazi ya kimataifa. Leo hii, wanafunzi wa kike wanashiriki kwa njia ya utayarishaji wa maudhui ya vyombo vya habari, kuchapisha makala na kuendesha makongamano ya kielimu, hivyo kuwa na nafasi hai katika kusambaza elimu ya Kiislamu. Mabadiliko haya yanaonesha mwelekeo mpya katika kuunda upya nafasi ya wanawake katika sekta ya dini.

Hawza ya Qum Katika Karne Mpya: Muungano wa kisunna na Ubunifu
Hawza ya Qum, kwa kuingia katika karne mpya, inahitaji zaidi ya wakati mwingine wowote mageuzi katika mbinu za elimu na upanuzi wa mahusiano ya kielimu.

Baadhi ya njia zinazotarajiwa kuchukuliwa na hawza ya Qum ni:

Kujenga mifumo ya elimu ya kidijitali: Kufundisha masomo ya Kiislamu kwa njia ya mtandao ili kuwafikia hadhira wa kimataifa.

Kupanuwa mitandao ya utafiti kimataifa: Mwingiliano wa kielimu katika nyanja za falsafa ya Kiislamu, masomo linganishi na maadili ya kimataifa.

Kutanua mifumo ya kisasa ya ijtihadi: Kulinganisha fiqhi na changamoto mpya za kijamii na kisiasa ndani ya ulimwengu wa Kiislamu.

Kwa kutumia fursa hizi, hawza ya Qum haitaimarisha tu nafasi yake katika ulimwengu wa Kiislamu, bali pia itakuwa mojawapo ya nguzo kuu za mazungumzo ya kitamaduni duniani. Qum, zaidi ya kuwa mji wa kidini, ni kituo cha uzalishaji na usambazaji wa elimu ya Kiislamu. Kuwekwa kwa vituo vya kimataifa vya elimu, kulea maelfu ya wanafunzi kutoka duniani kote, na juhudi za kueneza elimu ya Kiislamu kimataifa, vyote vinaonesha athari pana ya hawza hii kwa fikra ya kidini katika ulimwengu wa Kiislamu.

Leo hii, hawza ya Qum siyo tu kituo cha elimu, bali ni mhimili mkuu wa kufasiri upya elimu ya Kiislamu, mwingiliano wa kielimu na kulinganisha maarifa ya kidini pamoja na mahitaji ya dunia ya sasa. Programu ya baadaye ya hawza hii ni muunganiko wa maarifa ya kisunna na kufanya mageuzi ya kisasa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha